Wakenya Wazilahumu Mahakama kwa Ufisadi

Raia wa Kenya wameelezea malalamiko yao kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya utendaji wa mahakama kufuatia visa vya kuwakama na baadae kuwaachiilia washukiwa.

Wakitumia #MkishikaTunawachilia, baadhi wanasema, hatua ya kuwaachilia huru washukiwa inaonyesha kuwa mahakama haisaidii katika vita dhidi ya ufisadi nchini humo.

Malalamiko haya yanakuja baada ya Waziri wa afya nchini Henry Rotich kuachiliwa kwa dhamana ya dola 150, baada ya kukana mashtaka 20.

Mshtaka dhidi ya Rotich yanatokana na uchunguzi wa polisi kuhusu matumizi mabaya ya fedha katika miradi miwili ya mabwawa magharibi mwa taifa hilo ambayo yalikuwa yakisimamiwa na kampuni moja ya Italia kwa Jina CMC Di Ravenna.


Mabwawa hayo mawili yalipangiwa kugharimu dola bilioni 46 lakini wizara ya fedha chini ya usimamizi wa bwana Rotich ilikopesha bilioni 63 badala yake , alisema Noordin Hajj siku ya Jumatatu hivyo basi kuongeza deni kubwa la Kenya ambalo linadaiwa kufikia asilimia 55 ya mapato ya taifa hilo.

Baadhi ya Wakenya wanaona kuwa licha ya juhudi zinazofanyika kukabiliana na ufisadi nchini mwao, mahakama hazionyeshi ushirikiano katika kuwashughulikia kisheria wahusika.

Mfano katika ukurasa wa Twitter, Ali kere anasema mahakama nchini Kenya ni tatizo katika kukabiliana na ufisadi:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad