Wanaume Hawana Dogo....Wampachika Mimba Rapper Chemical na Kumkimbia



Rapa wa kike nchini mwenye muonekano wa kiume Chemical akiongea na Times Fm amekiri kuwa ana mimba ya miezi saba ya mwanaume ambaye sio wa Dar ndio maana amekuwa kimya kimuziki na pia hapost picha mpya instagram.

Chemical amesema Mwanaume huyo aliyempa mimba amemkimbia ndio sababu kila siku amekuwa akisema atajioa kwa sababu ndiye mwanaume aliyekuwa anamtegemea kuwa angemuoa.

Chemical amesema kuolewa muda ukifika ni lazima. Lakini amesema yeye Hana time kabisa na mwanaume anayemjia na sound za kumbadilisha kimuonekano.

Chemical amesema anajikubali alivyo Hana muda wa kusubiri wa kumbadilisha ikitokea ni maamuzi yake Kama alivyoamua sasa.

Chemical ameongeza kuwa hapendi wanaume wenye miili ya wabeba vyuma wala wanaume wanene au wenye furushi la kitambi, yeye anataka mwanaume mwenye mwili sinple tu wa kawaida

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad