App ya wapenzi wa jinsia moja Jack'd italipa kiasi cha pauni 189,000 baada ya picha za wapenzi wa jinsia moja kuvuja
Mtu yeyote ambaye ana nia ya kuzipata aliweza kuzipata picha hizo zilizovuja hata kama mtu huyo hana anuani ya Jack'd.
Mwanasheria mkuu wa New York Letitia James amesema app hiyo imeingilia faragha za watumiaji.
Watu wanaomiliki app hiyo, walishindwa kutatua tatizo lililojitokeza kwa mwaka mmoja baada ya kuonywa na watafiti.
Watafiti wa masuala ya uhalifu mitandaoni Oliver Hough waliripoti dosari kwenye app hiyo mwezi Februari mwaka 2018 lakini Kampuni ilishughulikia mwezi Februari mwaka 2019.
Bi James alisema: ''app inaweka'' taarifa nyeti na picha za faragha za watu kwenye hatari ya kuonekana kiholela na kampuni haikufanya chochote kwa mwaka mzima, kwa malengo kuwa waendelee kupata faida.''
Mabalozi wa Marekani waunga mkono wapenzi wa jinsia moja
Wapenzi wa jinsia moja wapigwa kwa kukataa kupigana busu
Mwanasheria huyo amesema amekubaliana na wamiliki wa app, kulilipa jimbo la New York kiasi cha pauni 189,000.
Pia imeahidi kutengeneza ''programu maalumu ya usalama'' kuwalinda watumiaji wake.
Jack'd imekuwa ikipakuliwa zaidi ya mara milioni tano kwenye Google Play.
Huwafanya watu wa app hiyo kuwa na uwezo wa kuweka picha zao ''binafsi'', kwenye ukurasa wa mbele ili ziweze kuonekana kwa watu maalumu wanaotaka kushiriki nao taarifa.
Hatahivyo, mwanaharakati Oliver Hough alibaini kuwa picha zote zilizotolewa kwenye app ziliwekwa kwenye server ya wazi na kufanya picha hizo kuwa wazi.
Mwezi Februari,BBC iliona ushahidi kuhusu picha za faragha bado zikiwa wazi kwenye tovuti.
''Waliona ripoti lakini walinyamaza kimya hawakufanya chochote,'' Bwana Hough aliiambia BBC News.
''Mwandishi wa habari aliwasiliana nao mwezi Novemba na wakafanya hivyohivyo.''
Wapenzi wa Jinsia Moja Kulipwa Baada ya Picha Zao Kuvuja
0
July 01, 2019
Tags