Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola Lugola ametoa onyo kali kwa MaRTO Mikoa ya
Morogoro na Mara akiwataka wachukue fursa ya kujitathimini katika utendaji wao kabla hajawachukulia hatua.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mji wa Malinyi, Mkoani Morogoro, leo, Lugola amesema yeye hatoi maagizo ya kisiasa bali anatoa maagizo yatakayomsaidia rais
kazi zake kwa wananchi wanyonge wanaopambana na umaskini na ajira.
Read More: Nafasi za Ajira 59 Zilizotangazwa Leo
“Wapo baadhi ya askari waonevu, wanaendelea kuchukua rushwa, wajitathimini, katika utendaji wao kabla sijawachukulia hatua kali za kinidhamu,” alisema Lugola.
Lugola katika hotuba zake katika mikutano yake mbalimbali alisema Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na haitaki kumnyanyasa mwananchi yeyote kupitia makosa ya trafiki wasiokuwa waaminifu.
Lugola alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi nchini, kuwa bodaboda zinazotakiwa kuwepo kituo cha polisi ni zile zilizopo katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali.
“Bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,” alisema Lugola.
Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Malinyi na Tanzania kwa ujumla wafuate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa.
Pia Waziri Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya askari Polisi hapa nchini kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za Jeshi, anasema kwa kufanya hilo kunaleta kero kwa madereva na pia anayekamatwa anaweza akadhaniwa kuwa ni jambazi.
Lugola anaendelea na ziara yake mkoani Morogoro, na anatarajia kumaliza ziara hiyo Wilaya ya Ulanga Mkoa humo
Read More: Nafasi za Ajira 59 Zilizotangazwa Leo