Waraka wa Kinana na Makamba Wadau Waunga Mkono Musiba Ashughulikiwe


Wadau wa mitandao ya kijamii wameunga mkono salakata la Makatibu Wastaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba na Abdulrahman Kinana dhidi ya Cyprian Musiba kuwa ashughulikiwe.

Jana viongozi hao wametaka achukuliwe hatua Musiba  dhidi ya tuhuma anazozitoa za uzushi badala ya kuendelea kukingiwa kifua.


Viongozi hao wastaafu katika tamko lao walilolitoa jana walisema wanashangazwa kwanini Musiba achukuliwe hatua licha ya kwamba anatumia lugha za vitisho na kuhatarisha usalama wa raia hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yake.

Walisema kwa muda mrefu amejitokeza mtu anayejitambulisha kama ni mwanaharakati na mtetezi wa Rais John Magufuli na kuwatuhumu kwa mambo ya uzushi na uongo.

“Tumetafakari kwa kina na kuamua kutoa taarifa hii kwa umma kuhusiana na Musiba dhidi yetu. Watanzania wanajua haya anayoyasema mtu huyu kuhusu watu mbalimbali sio ya kwake anatumwa kutekeleza maagizo na kutumika kama kipaza sauti tu. Huyu ni mamluki anayetumika kuivuruga CCM na nchi yetu katika mazingira haya hatuwezi kukaa kimya,”

“Tunasikitika kwamba Musiba licha ya kuwatuhumu na kuwakashfu Watanzania wenzake, viongozi na watendaji kwenye serikali, kwenye taasisi kadhaa za umma za kijamii n ahata kwenye sekta binafsi ameachwa akitamba jambo linaloashiria kwamba anakingiwa kifua. Hata anapotoa lugha za vitisho na za kuhatarisha usalama wa raia hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yake,”

Wamesema mara kadhaa watanzania wanajiuliza huyu Musiba anatumwa na nani? Pili anakingiwa kifua na nani? Tatu anatumika kwa malengo gani? Na nne nini hatima ya mikakati yote?

Viongozi hao wastaafu wamesema tafakari yao inawapa majibu haya kuwa mtu huyu anatumiwa na watu wenye uwezo wa kumlinda na kumkingi kifua bila kuhojiwa na taasisi yoyote wala na mtu yoyote.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Muusiba ni Mzaalendo na ni Mkereketwa.
    mengianayo sema yuko Sahihi.
    Mpaka mnajibu ni kweli yana wahusu kikweli.

    MUsiba endelea mwanangu na Harakati za kumuuga mkono Kipenzi chetu JPJM.
    mungu akulindeeni IshaaAllah

    ReplyDelete
  2. big up musiba endelea husiwasikilize hivyo vizee..ukweli unauma

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad