Watano wanaswa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Watanzania 9 nchini Msumbiji, Mmoja afariki Dunia


Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema kuwa watu watano wanaoshukiwa kuhusika na tukio la mauaji ya Watanzania 9 nchini Msumbiji, wanashikiliwa na vyombo vya dola nchini.


IGP Sirro amesema hayo Jana Julai 15, 2019 katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za polisi mkoani.

“Katika tukio la Msumbiji, niliahidi kwa Watanzania kuwa waliofanya hilo tukio, damu ya Watanzania haipotei bure. Mpaka sasa watu watano wamekamatwa na mmoja wao ametangulia mbele ya haki na wanatajana,” amesema IGP Sirro.

Akieleezea zaidi kuhusu washukiwa hao, IGP Sirro amesema mtuhumiwa mmoja kati ya watano waliokamatwa amefariki dunia.

IGP Sirro amesema mpango wa utekelezaji wa tukio hilo ulisukwa hapa nchini, huku utekelezaji wake ukifanyika nchini Msumbiji.

“Inaonekana mipango yote ilifanyika nchini kwetu, tukio lilifanyika Msumbiji. Kimsingi wote wamepatikana wanaendelea kutajana, operesheni inafanyika kwa kushirikiana na wenzetu wa Msumbiji,” amesema IGP Sirro.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad