Watu wasiopungua 35 wamefariki na wengine 101 kujeruhiwa baada ya lori ya mafuta ya petroli kulipuka kusini mwa Nigeria.
Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu katika kijiji cha Ahumbe katika jimbo la Benue, wakati lori hilo lililokuwa limepoteza udhibiti na kuanguka lilishika moto huku watu kadhaa wakijaibu kuchota mafuta yaliyokuwa yakivuja,kulingana na taarifa iliyotolewa na Aliyu Baba, kamanda wa serikali wa Shirikisho la Usalama wa barabara (FRSC).
Watu hao walichota mafuta kwa muda wa dadika 45 hadi wakati basi aina ya toyota lilipogonga lori hilo na kusababisha mlipuko wa kwanza ambapo watu 14 waliokuwa kwenye basi hilo walifariki papo hapo. Mlipuko wa pili ambao ulisababisha vifo vingi ulifanyika dakika chache tu baadaye.