Waziri Bashungwa ataka vifungashio kwa wafanyabiashara ndogo

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amevitaka viwanda kutengeneza vifungashio vidogo kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo kwani wajasiriamali wana uhitaji mkubwa wa vifungashio hivyo.

Bashungwa aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea kiwanda cha A to Z pamoja na kiwanda cha Sunflag kwa lengo la kusaidia viwanda kwa kutangaza masoko, kuangalia mazingira ya kufanya kazi pamoja na kusaidia ajira kwa vijana na akinamama ili kuendelea kuinua ajira viwandani.

Alipokuwa kiwanda cha A to Z aliwataka wazalishe kwa wingi vifungashio vidogo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo kwa sababu vifungashio hivyo bado ni changamoto wafanyabiashara hao pamoja na gharama kuwa kubwa, hivyo wakitengeneza vifungashio hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuendesha biashara zao.

Alisema kwa viwanda vinavyotengeneza nguo kuna umuhimu mkubwa wa kuvikuza kwa ajili ya kuinua biashara ya pamba pia kuhakikisha bidhaa zinazotengenezwa watanzania wanatumia bidhaa zao.

"Tunapaswa kupenda vitu vya nchini kwetu na si kuvibeza huku nchi nyingine zikitumia bidhaa zetu vizuri kuliko hao wengine," alieleza.

Hata hivyo, alipongeza viwanda hivyo alivyotembelea kwa ufanisi wao mzuri wa kazi pamoja na mikakati yao walioipanga katika kuhakikisha wanainua biashara ya bidhaa zao.

Pia alitoa rai kwa viongozi kuhakikisha wafanyakazi katika viwanda hivyo malipo yao yanalipwa kwa wakati bila kuwa na changamoto yeyote na kuangalia kwa upande wa muda wanaoingia na kutoka ili wasinyonywe kwa namna yoyote ile.

Mkurugenzi wa kiwanda cha A to Z, Jayant Shah alisema wanamuunga mkono Waziri huyo kwa kufanya jitihada ya kutengeneza vifungashio vitakavyokidhi mahitaji ya wafanyabiashara ndogo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad