Waziri Kigwangalla Akubali Yaishe, Adai Watarekebisha Sanamu ya Nyerere Baada ya Wadau Kupaza Sauti


Waziri wa Maliasili na Utali, Dk Hamis Kigwangalla amesema watakwenda kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika picha ya sanamu iliyochorwa ikimuonyesha Mwalimu Julias Nyerere ambayo imeleta gumzo katika mitandao ya kijamii.

Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa imeonyesha ni jinsi gani vijana wa kisasa kuijua vizuri taswira ya Mwalimu Nyerere, hivyo watawatumia wataalamu kurekebisha mapungufu yalitojitokeza.

Kupitia ukuraha huo Kigwangalla aliandika ujumbe unaosomeka”Kitu kikubwa kilichonifurahisa ni kuwa kizazi cha vijana wa kisasa kabisa bado kinakumbuka vizuri baba wa Taifa, kinamuenzi na kumheshimu sana na ndio maana wanaikumbuka taswira yake. Tutatumia vizuri zaidi Wataalamu wetu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kabla ya kuitumi,”



Picha hiyo ya sanamu ambayo iliwekwa katika uzinduzi wa hifadhi ya Burigi – Chato mkoani Geita ilizua mjadala katika mitandao ya kijamii huku wengine wakihoji huyo ndiye Nyerere anayejulikana ama ni mwingine wa Chato.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad