Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May kuongoza kikao cha dharura dhidi ya Iran

Waziri mkuu wa Uingereza ataongoza kikao cha kamati ya dharura siku ya Jumatatu baada ya meli ya mafuta iliokua ikipeperusha bendera ya Uingereza kukamatwa na Iran katika Ghuba.

Theresa May anatarajiwa kupokea taarifa kutoka kwa mawaziri na maafisa na kuzungumzia umuhimu wa kuzipatia usalama wa kutosha meli katika eneo hilo.

Hatua hiyo inajiri kufuatia ripoti kwamba mawaziri wanapanga kupiga tanji mali ya Iran.


Waziri wa maswala ya kigeni Jeremy Hunt anatarajiwa kuwajuza wabunge baadaye kuhusu hatua ambazo seriikali ya taifa hilo itachukua.

Siku ya Jumapili , afisi ya wizara ya maswala ya kigeni ilithibitisha kwamba bwana Hunt alizungumza na wenzake wa Ujerumani na Ufaransa ambao wote wameshutumu vitendo vya Iran.

Bwana Hunt aliwashukuru mawaziri wa maswala ya kigeni Jean Yve Le Drian na waziri wa kigeni nchini Ujerumani Heiko Maas kwa kuunga mkono Uingereza.

Mawaziri wote walikubaliana kwamba kuna umuhimu wa kuimarishwa kwa usalama katika eneo hilo ili meli kuweza kupita katika mkondo wa bahari wa Hormuz kwa usalama huku ikizuia hatari yoyote ya mgogoro kutibuka katika eneo hilo.


Mawaziri wamekana madai kwamba serikali imepuuza hali inayoendelea katika eneo la Ghuba kutokana na siasa za nyumbani.

Chansela Phillip Hammond amesisitiza kuwa serikali imekuwa ikifanya mazungumzo na Marekani pamoja na washirika wake wa Ulaya ili kujibu vitendo vya Iran katika kipindi cha miezi kadhaa.

Na waziri wa ulinzi Tobias Ellwood alisema kuwa Uingereza ilikuwa na meli ambazo zimekuwa zikipitia mkondo huo kila siku na kwamba ni vigumu kuzisindikiza meli zote.

Alipendekeza kwamba fedha zaidi zinafaa kuwekezwa katika jeshi la wanamaji wa Uingereza ili kuliwezesha kushiriki vyema katika ulingo wa kimataifa.

Je wanasiasa wa Uingereza wanasema nini?
Akizungumza katika kipindi cha BBC , bwana Hammond alisema kwamba Uingereza itatumia kila njia ya kidiplomasia ili kutatua mzozo huo.

Alisema kwamba vikwazo , ikiwemo vile vya kifedha dhidi ya Iran tayari vimewekwa na haijajulikani ni nini zaidi kinachohitajika kufanywa.

Lakini bwana Dancun Smith aliambia BBC kulikuwa na maswali ambayo yalihitaji kuulizwa kuhusu vitendo vya seriikali ya Uingereza.

Alisema kwamba kuzuiliwa kwa meli ya mafuta ya Iran wiki mbili zilizopita kulifaa kuwa onyo kwamba meli za Uingereza zinazopitia Ghuba zilihitaji kupatiwa usalama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad