Waziri Mwakyembe akerwa na kiburi cha viongozi wa TFF, ‘Kama wanaiga Misri na wao wajiuzulu’



Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai yake kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Soka nchini TFF kumtimua kocha Emmanuel Amunike

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa kama TFF wameamua kufuata nyayo za Misri katika kumfuta kazi Amunike basi na wao wanapaswa wakamilishe mchakato kwa kujiuzulu nafasi zao.

”Sisi hatuna tatizo na maamuzi ya TFF endapo tu yatatupeleka mbele, lakini kama ni uamuzi wa kuwaiga Wamisri baada ya kutolewa AFCON, hayo ni makosa makubwa sana kwa sababu kama unaiga basi nao wakamilishe kwa kujiuzulu safu nzima ya uongozi”, amesema Waziri Mwakyembe.

Aidha, amesema kuwa ubabaishaji katika soka hawezi kukubaliana nao ambapo amesema ni bora kuishia kucheza karata kuliko kuingia kwenye soka la ubabaishaji na kuingia kwenye mipango ya hovyohovyo na wanaoharibu hakuna anayewajibika.

Pia amesema kuwa hadi kufikia 24 Julai mwaka huu, benchi la ufundi la Taifa Stars na Viongozi wa TFF wanatakiwa kutoa ripoti yao ya michuano ya AFCON kwa ajili ya kujadiliwa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waziri wangu usimtetee sana kocha kwani nakushauri kaa na wachezaji mmoja mmoja wakuambie kuhusu kocha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad