Waziri wa Fedha Kenya Henry Rotich Akamatwa kwa Tuhuma za Ufisadi

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich amejisalimisha kwa maafisa wa upelelezi hii leo, muda mfupi baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini kuagizwa akamatwe.

Kwa mujibu wa Nairobi News, Waziri Rotich alipelekwa kwa gari hadi katika makao makuu ya idara ya upelelezi ambako anahojiwa kuhusu malipo yaliotolewa kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini.

Anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa.

Hapo awali, mkurugenzi wa mashtaka Kenya aliagiza kukamatwa kwa waziri wa fedha Henry Rotich na ashtakiwe kuhusu ufisadi

Mkurugenzi huyo wa mashtaka Noordin Haji amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kumshtaki waziri wa fedha Kenya Henry Rotich, na maafisa wengine wa serikali kuhusu kandarasi zilizotolewa kwa kampuni ya Italia kujenga mabwawa mawili.

Washukiwa wa ufujaji wa pesa Kenya wafikishwa kortini
Maafisa wakuu wakamatwa katika kashfa ya rushwa Kenya
Jinamizi la ufisadi limemshinda nguvu rais Kenyatta?
Noordin Haji ameeleza kwamba watashtakiwa kwa "kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi" miongoni mwa mambo mengine.

Mashtaka hayo yanahusiana na ujenzi wa mabwawa mawili nchini uliogharimu fedha nyingi.

Haki miliki ya pichaKTN
Mnamo Machi Waziri Rotich alikana kupitia tangazo kubwa kwenye gazeti nchini kufanya makosa yoyote.

Kampuni hiyo ya Italia CMC de Ravenna pia imekana tuhuma hizo.

Umuhimu wa uadilifu kwa mujibu wa katiba
"Katiba yetu inasisitiza baadhi ya maadili yetu yakiwemo uadilifu… kuyatimiza hususan kwa walio uongozini..."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad