Waziri wa utalii akamatwa kwa utakatishaji fedha


Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Zimbabwe (ZACC), imemkamata Waziri anayeshughulikia masuala ya mazingira na utalii, Prisca Mupfumira akidaiwa kuhusika katika utakatishaji wa fedha.


Fedha zilizokamatwa

ZACC hivi karibuni imepewa kibali cha kukamata watuhumiwa nchini humo, ambapo imeanza na Waziri huyo ambaye anadaiwa kuhusika katika utakatishaji wa kiasi cha Dola za Kimarekani millioni 95.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Justice Loice Matanda-Moyo amethibitisha kuwa Waziri huyo amekamatwa jana, Julai 25 na atafikishwa mahakamani leo, Julai 26.

"Bado yuko nasi na anatarajiwa kufikishwa kortini kesho (leo). Anakabiliwa na mashtaka ya rushwa yanayojumuisha dola milioni 95. Baadhi ya makosa hayo ni hutokana na ukaguzi wa NSSA, anadaiwa alifanya makosa mengine katika wizara yake ya sasa (Wizara ya Mazingira, Utalii na Ukarimu)", amesema Justice Matanda Moyo.

Hivi karibuni, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa aliwachagua wajumbe wapya 12 wakiongozwa na Justice Loice Matanda-Moyo na kuwapa mamlaka ya kukamata washukiwa wa rushwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad