Yanga SC yawaleta AS Vita siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi

Kuelekea kilele cha wiki ya mwananchi Klabu ya Yanga inawaleta AS Vita kutoka nchini Congo kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki katika siku hiyo.

Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Fredrick Mwakalebela amesema kuwa ziara ya wiki ya mwananchi itaanza Julai 28 mwaka huu na kilele chake kitakuwa Agosti 4 mwaka huu.

Sherehe hizo za kilele cha wiki ya mwananchi zitafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad