Yemen: Watoto Milioni 1.8 wanakabiliwa na Utapiamlo
0
July 31, 2019
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Yemen vimesababisha mateso ya kusikitisha kwa watoto wa nchi hiyo. Zaidi ya watoto milioni 1.8 wanakabiliwa na utapiamlo katika nchi hiyo ambapo karibu asilimia 45 ya hospitali zimeharibiwa na vita.
Wazazi wanalazimika kusafiri na watoto wao kilomita kadhaa kwenye barabara mbaya ili kupata angalau hospitali ambazo zingali zinahudumu huku wakiwa wanakabiliwa na hatari ya kuuawa kwenye safari hiyo.
Kufikia leo, vita hivyo ambavyo vilizuka mwaka wa 2015 vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 10,000 huku wengine milioni 3 wakitoroka makwao, hii ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa. Zaidi ya watu milioni 25 nchini Yemen wanakabiliwa na hatari ya njaa au kifo kutokana na magonjwa yanayotokana na ukosefu ya maji masafi ya kunywa.
Tags