Zaidi ya watu 40 wameuawa nchini Afrika Kusini juma lililopita
0
July 19, 2019
Wanajeshi nchini Afrika Kusini wanafanya doria kwenye mitaa ya viunga kadhaa vya mji wa Cape town, ambavyo vimekuwa vikikumbwa na vurugu za magenge ya watu.
Zaidi ya watu 40 wameuawa mwishoni mwa juma lililopita.
Hatua hii imelenga kusaidia polisi kupambana dhidi ya wimbi la ongezeko la vitendo vya mauaji.
Wanajeshi wenye silaha waliwasili na magari yao ya kijeshi siku ya Alhamisi na kuanza kufanya operesheni ya ukaguzi katika eneo la Manenberg, eneo linadaiwa kushamiri kwa ghasia.
Vikosi vya kijeshi vitapelekwa kwenye maeneo 10 ya mji wa Cape town.
A.Kusini: Jeshi lapelekwa Cape Town kuyakabili magenge
Kwanini idadi ya watu inaongezeka Uganda?
Takwimu kutoka kwenye nyumba za kuhifadhia miili zinaonyesha ongezeko la vifo katika eneo hilo, huku kukiwa na ripoti ya vifo vya watu 1,000 mwaka huu pekee.
Mwezi uliopita, askari sita waliokuwa kwenye kikosi cha kupambana na magenge yanayofanya vurugu walijeruhiwa vibaya wakiwa kwenye doria.
Hii si mara ya kwanza vikosi vya kutuliza ghasia vinaingia mtaani. Miaka minne iliyopita, Jeshi, likiwa limeambatana na polisi na idara nyingine za serikali katika operesheni ya kupambana na uhalifu.
Lakini wakosoaji wa mambo wanasema jeshi si suluhu ya ghasia zinazokumba maeneo kadhaa ya Cape town kwa miaka kadhaa sasa.
Tags