Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ameituhumu Marekani kwa kuanzisha kile alichokiita ugaidi wa kiuchumi.
Zarif ameyasema hayo jana jumatano alipoutembelea Umoja wa Mataifa nchini Marekani ambapo nchi hiyo ilimwekea haraka vikwazo vya kuzuia mienendo yake.
Waziri huyo wa mambo ya kigeni, aliingia mjini New York, kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo endelevu na kusema kuwa raia wa Iran wanakabiliwa na Ugaidi wa kiuchumi wa Marekani inayotaka kutimiza lengo la kisiasa lililo kinyume na sheria.
Kufuatia mvutano huo, Umoja wa mataifa umeeleza hofu yake juu ya vikwazo vilivyowekwa na Marekani kwa Zarif, wakati nchi hiyo ikitegemewa kusimamia mahudhurio ya kidiplomasia ya Umoja wa Mataifa.