Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anakwenda kukabidhi ushahidi wa mfanyabishara Raphael Onyangi, sehemu alipo ili aweze kuachiwa.
Zitto amesema hayo leo kuwa wanatambua Onyangi alipo na wanataka aachiwe mara kwani taarifa zake wanazo alipofishwa.
Alisema kwa msaada waliokuwa nao pamoja na watu waliowatumia wamefanikiwa kujua Onyangi alipohifadhiwa.
‘Tunaomba wamuachiae kabla ya sisi kwenda kuomba msaada sehemu nyingine na kwenda kumfuata alipo lengo tutakomesha vitendo hivyo ni mambo ambayo yanahitaji ujasiri sasa itafika wakati tutasema basi lazima tuseme,” alisema Zitto.
Aliongezea kuwa:“Naiomba serikali ya Kenya iitake serikali ya Tanzania imuachia raia wao serikali zenyewe zinajua namna ya kufanya mazungumzo baina yao. Sisi tutaikabidhi serikali ya Kenya ushahidi wa kila mahala alipokuwa Raphael ili tuiache serikali ya Kenya ione cha kufanya kwa mazungumzo na serikali ya Tanzania tutaukabidhi leo Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ili kuona namna bora ya kumuokoa raia wao maana ni jukumu lao kulinda raia wao kokote alipo duniani,”
Aidha, Ziito ameiomba jamii ya kimataifa kukemea vikali matendo yanayoendelea nchini dhidi ya wanasiasa wa upinzania kwani matendo hayo yana madahara makubwa.
Mfanyabiashara huyo ambaye ni raia wa Kenya anaishi nchini alitekwa na watu wasiojulikana wiki iliyopita akiwa na mkewe eneo la Oysterbay huku wakiwa na mitutu ya bunduki na kumshusha katika gari yake na kuondoka naye .