Zuma Arejea Katika Uchunguzi wa Mahojiano Kuhusu Rushwa

Zuma arejea katika uchunguzi wa mahojiano kuhusu rushwa
Wakili wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ameiambia tume ya uchunguzi ya madai ya ufisadi kwamba mteja wake asingeliweza kushiriki tena mahojiano na tume hiyo kwa sababu anaamini kuwa hatendewi haki kwenye mahojiano hayo.

Wakili Muzi Sikhakhane ameaiambia tume hiyo ya uchunguzi mapema leo hawataendelea kushiriki vikao vya uchunguzi, kwani Zuma amekuwa muhanga wa maswali ya kuchafua na kuudhi.

Zuma alikuwa anatarajiwa kurejea katika uchunguzi wa serikali kuhusiana na rushwa leo Ijumaa, akiwa tayari ameshahudhuria mahojiano hayo katika siku tatu za kutoa ushahidi katika uchunguzi huo wiki hii, kabla ya mawakili wake kuomba kuahirishwa kwa mahojiano hayo.

Uchunguzi huo, ambao Zuma alikubali kuunda katika wiki za mwisho za utawala wake, unaangazia madai ya ufisadi pamoja na matumizi ya ushawishi ambayo yalikuwapo katika utawala wake wote wa miaka tisa madarakani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad