Afungwa miaka 20 jela kwa kuweka Mabomu kwenye bahasha na kutuma kwa viongozi


Mwanaume ambaye mwaka wa 2018 aliweka mabomu kwenye bahasha na kuvituma kwa viongozi mashuhuri wa kisiasa nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani na mahakama mjini New York.

“Nasikitika sana kwa kile nilichofanya,” Cesar Sayoc aliambia jaji Jed Rakoff kabla ya kusomewa hukumu yake. Sayok mwenye umri wa miaka 57 kutoka jimbo la Florida alituma bomu 16 kwa watu 13 mashuhuri mwaka jana na kusababisha hofu kwote nchini Marekani.

Miongoni mwa aliyowalenga ni pamoja na rais mstaafu Barack Obama, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton miongoni mwa wanasiasa wengine ambao wanapinga sera za rais wa sasa Donald Trum.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad