Ajali ya Morogoro: Majeruhi Mwingine Mmoja Afariki
0
August 17, 2019
IDADI ya vifo kutokana n ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kuwaka moto mkoani Morogoro, imeongezeka na kufikia 94 baada ya majeruhi mwingine mmoja kufariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa MNH, Aminiel Aligaesha, imesema idadi ya majeruhi wanaopatiwa matibabu sasa ni 20.
Tags