Ajinyonga Baada ya Ndugu Kukataa Kumchangia Hela ya Kumzika Mkewe


Mkazi wa kijiji cha Kilwa Wilayani Rombo, Ambros Gervas Marandu (54) amekutwa amejiua kwa kujinyonga kwenye mwembe uliopo nje ya nyumba yake

Polisi imeeleza kuwa chanzo cha Ambros kujinyonga ni kutokana na ndugu zake na ndugu wa mke wake kukataa kumchangia fedha ili amzike mke wake

Ambros alimuuguza mke wake kwa muda mrefu na baada ya mkewe kufariki aliwaambia ndugu wa mke lakini ndugu hao walimwambia wanataka mchango wake

Ambros aliwajibu ndugu hao kuwa yeye hana fedha kwani amemuuguza mkewe kwa muda mrefu. Alipowaomba mchango ndugu zake walimjibu "Wewe mzike tu mwenyewe"

Polisi imeeleza kuwa, inavyoonekana Ambros alikosa msaada wa kimawazo na upendo umepungua kwenye jamii, kwani alipoomba ndugu zake auze kihambaa ili amzike mkewe, ndugu hao walikataa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad