Albert Msando amlipia Rais Magufuli deni Muhimbili


Alberto Msando ambaye ni Wakili wa kujitegemea amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kulipa MILIONI 5 ambazo Rais John Magufuli aliahidi kuzitoa kumlipia Mama aliyemlilia akitaka alipiwe gharama hizo ili apatiwe mwili wa Mama yake.

Baada ya kumsaidia rahisi kulipa kutoka katika mfuko wake Alberto Msando Ameandika Haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Albertomsando
Leo tarehe 23.08.2019 nimekabidhi Sh. 5,000,000 kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni michango ya wananchi waliojitolea kumchangia Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli kulipa deni ambalo alijitolea kulipa kwa ajili ya marehemu Sabina Kitwae Loita. Deni la sh. Laki Tatu iliyobaki atalipa Mh. Rais mwenyewe. Waliochanga ni watanzania wa kawaida ambao walitoa sh 1,000 au 2,000 kwa kutuma kwenye simu. Nawashukuru wote ambao walituma fedha zao na zimekabidhiwa. Nawashukuru wale ambao walipinga zoezi hili kwani wamenipa nafasi ya kujifunza kuhusu upokelewaji wa wazo na tafsiri. Kikubwa tujifunze 1. Matumizi bora ya mitandao na nafasi zetu. 2. Mh. Rais ni binadamu mwenye moyo na hisia kama mimi na wewe. Anastahili kupewa moyo na kusaidiwa katika kutekeleza majukumu yake 3. Wenye shida ni wengi usisubiri mpaka fulani aanzishe kuchangia ndio uchange au upinge michango. Nawashukuru wote na Mungu aendelee kuwabariki. 🙏🏿🙏🏿


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad