Aliyeitungua Yanga uwanja wa Uhuru afunguka

 

Mshambuliaji wa Ruvu Shooting Sadat Mohamed, amesema kuwa amefurahi kuipa ushindi leo timu yake ya Ruvu Shooting mbele ya mabingwa wa kihitoria Yanga. 


Akizungumza mara baada ya mchezo, Mohamed amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kufikia hapo kutokana na ushindani mkubwa ambao ulikuwepo kwenye mchezo wa leo. 


"Tumepambana mwanzo mwisho na mchezo ulikuwa mgumu mwisho wa siku tumepata ushindi na pointi tatu kwetu ni jambo la msingi na la furaha sana. 


"Ushirikiano ambao tumekuwa tukiufanya na namna ya mazoezi ambayo tumeyafanya yametusaidia kutupa ushindi mbele ya Yanga leo tutazidi kupambana na siri ya ushindi ipo kwenye ushirikiano," amesema. 


Ruvu Shooting msimu uliopita ilipigwa na Yanga nje ndani leo ni mara ya kwanza kusepa na pointi tatu mbele ya Yanga uwanja wa Uhuru.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad