Aliyemuua Mkewe Kwa Kumchoma na Magunia ya Mkaa Ataka Apatiwe Fedha zake zilizokuwa Kwa Simu


Aliyemuua mkewe kwa kumchoma na magunia ya mkaa ataka apatiwe fedha zake zilizokuwa kwa simu
Posted On: August 27, 2019 11:21 Am GMT+0000  Posted By: Beatrice  Comments: 0
Mfanyabiashara Hamis Said (38), anayekabiliwa na kesi ya kumuua mkewe, Naomi Marijani ameieleza Mahakama ya Hakimu Kisutu kuwa anaomba apatiwe Line zake mbili za simu zenye zaidi ya Sh.Milioni 5 kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya nyumbani kwake pamoja na kumlipia ada mwanae.

Said ambaye hivi karibuni alitoa vitisho kwa Waandishi wa Habari kwamba atawafanya kitu mbaya ametoa maombi hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.

Kabla ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali Wankyo Simon amemueleza Hakimu Ally kwamba shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo, Said alinyoosha mkono na kumeleza Hakimu kwamba ana mambo mawili muhimu ikiwemo nakala yake ya Hati ya Mashitaka na Line zake za simu zilizopo Central Police.

Amedai kuwa anaomba apatiwe line zake mbili zenye zaidi ya Sh.Mil 5 ili ziweze kutumika kwa matumizi madogo madogo pamoja na ada ya mwanae.

“Sitaki simu ila nipatiwe line ambazo nimpatie ndugu yangu atoe hizo hela kwa ajili ya matumizi, ikiwezekana zitolewe hata Polisi wakiwepo,”amesema.

Baada ya kueleza hayo, Wakili Wankyo ameeleza kuwa hawawezi kumpatia line hizo kwa sababu simu ni sehemu ya upelelezi.

Pia ameeleza kuwa kama anahitaji fedha hizo aandike barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10, 2019.

Mshitakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ambapo adaiwa alilitenda Mei 15, 2019 katika oneo la Geza Ulole Kigamboni Dar es Salaam ambapo alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.

Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad