Atakayempa simu mtoto chini ya miaka 18 kukiona - Nditiye
0
August 26, 2019
Na Clavery Christian Kagera.
Naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano muhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa usajiri wa laini za simu kwa alama za vidole umezidi asimilia 70% na kwamba zoezi zinaenda vizuri.
Akizungumza na Muungwana Blog Naibu waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano mh, Atashasta Nditiye amesema kuwa serikali inataka wanachi wafurahie huduma ya mawasiliano bila kuwa na tatizo lolote ambapo amesema kuwa mawasiliano yanachangia kwa asilimia kubwa pato la taifa na yameraisisha shughuli za kiuchumi na shughuli za kiusalama wa nchi.
"Tunahitaji watu wawe na laini chache chache kabisa anazozitumia ili sisi kama serikali tujue anayezitumia huyo ni nani, tunataka kuepukana na zile sms za nitumie hiyo hela kwenye namba hii na watanzania wanatuma kwasababu unakuta mtu mwingine anashida labda anauguza unakuta anatuma hiyo hela kumbe anaibiwa sasa tunataka kila mtu anayemiliki laini ya cm tumtambue" Alisema Muhandisi Atashasta Nditiye.
Ameongeza kuwa watanzania wanawasiliana kwa asilimia 94% na asilimi 6% iliyobaki serikali tiali imehainisha maeneo hayo ambapo inakaribia kutangaza tenda kwa ajiri ya kupeleka huduma ya mawasiliano hayo katika maeneo ambayo hayana huduma ya mawasiliano kote nchini.
Mh, Nditiye amewaonya wazazi na walezi wanaowaruhusu watoto walioko chini ya umri wa miaka 18 kumiliki simu na lain za mawasiliano kinyume na sheria inavyosema, "sisi kama serikali tunasema mtu ambaye hajatimiza umri wa miaka kumi na nane haruhusiwi kumiliki simu maana hawezi kusajiriwa kumiliki ile simu na simu ili itumike lazima iwe imesajiriwa kwa jina la mtu mwingine huyo mwingine sasa huyo ndo tutakaye mkamata aliyemkabidhi simu huyo mtoto awe wa kiume au wa kike akakamatwa nayo ikamletea madhara tutaiweka kwenye system yetu tutaiangalia na tutajua ni nani na ndo tutakayeanza naye kama shaidi namba moja kulingana na madhara ambayo itakuwa umempatia huyo mtoto" Alisema Mh, Nditiye.
Zoezi la usajiri wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole lilianza rasmi tarehe 1 mei mwaka huu na linatarajiwa kukamilika tarehe 31 disemba mwaka huu.
Tags