Balinya, Tshishimbi Wafunika Utambulisho Yanga

Balinya, Tshishimbi Wafunika Utambulisho Yanga
MASTAA wa Yanga, straika Juma Balinya na kiungo Papy Tshishimbi, jana walishangiliwa kwa shangwe nyingi zaidi wakati majina yao yakitajwa kwenye utambulisho wa wachezaji katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Yanga jana ilitambulisha mchezaji mmojammoja kabla ya kuanza kwa mechi dhidi ya Kariobangi Sharks kwa kuwa nyota wake wengi ndiyo walikuwa wakionekana kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam wakiwa na uzi mpya wa Yanga. Sasa katika utambulisho huo, mastaa wote walishangiliwa lakini shangwe zaidi zilisikika baada ya majina ya Balinya, Tshishimbi kutajwa.

Wengine walioshangiliwa sana ni kipa Farouk Shikalo, mastraika Wanyarwanda Issa Bigirimana na Patrick Sibomana pamoja na winga Mrisho Ngassa ambaye Wanayanga wanamtazama kama mtoto wa nyumbani kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa klabu hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad