SERIKALI imekuja na mkakati wa kuundwa kwa mamlaka moja ya kusimamia sekta ya sanaa na ubunifu katika kuboresha na kuleta mageuzi katika sekta hiyo baada ya kuanzishwa kwa mkakati wa kuziunganisha taasisi zinazoshughulika na sekta hiyo ambazo ni Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Bodi ya Filamu na Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA).
Wasanii wa aina zote, watunzi na waandishi, wabunifu, waandishi wa habari na wadau wote wa sanaa wamekaribishwa katika mkutano wa kujadili mchakato wa uundwaji wa mamlaka hiyo.
Katika mkutano huo atakuwepo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison George Mwakyembe na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Innocent Bashungwa.
Mkutano huo utafanyika siku ya Jumatano, Agosti 28, 2019 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar kuanzia saa 3:00 asubuhi.
BASATA, COSOTA na Bodi ya Filamu Sasa Kuwa Chombo Kimoja
0
August 27, 2019
Tags