Bayern Munich yamsajili Coutinho kwa mkopo

Bayern Munich imemsajili mshambuliaji wa kiungo cha kati Philippe Coutinho kutoka Barcelona kwa mkopo msimu mpya inayojumuisha uwezekano wa kumnunua.

Barcelona inasema timu ya Ujerumani italipa Euro milioni 8.5 kumchukua mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo huku kukiwana fursa ya kumnunua kwa kititia cha Euro milioni 120.

Bayern pia italipa mshahara wa Coutinho katika kipindi kizima cha kucheza kwa mkopo.


"Kwangu mimi, mabadiliko haya yanaashiria changamoto mpyakatika nchi mpya katika mojawapoya vilabu bora Ulaya," amesema.

"Nalitazamia sana hili. Nina malengo makubwa, kama Bayern, na nina hakika naweza kulifanya hilo na wachezaji wenzangu. "

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mkurugenzi mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge ameongeza: "Tumekuwa tukishirikiana na Philippe Coutinho kwa muda sasa na tunafurahi sana kwamba tunaweza kutimiza uhamisho huu.

"Shukrani zetu kwa FC Barcelona kwa kukubali uhamisho huu. Tumepata mchezaji, Philippe, anayekuja FC Bayern atakayimarisha kameni yetu kwa ubunifu na mbinu zake imara."

Coutinho, aliyekuwa akitazama mechi ya La liga ya Barcelona'iliposhindwa na Athletic Bilbao siku ya Ijumaa, amejiunga kutoka Liverpool katika mkataba wa thamani ya pauni milioni 142 mnamo Januari 2018.

Licha ya kufunga mabao 21 katika mechi 76 kwa timu hiyo ya mabingwa Uhispani, hajafikia matarajio na amehusishwa na uhamisho kwenda katika klabu kadhaa msimu huu wa joto.

Inaaminika alijumuishwa kama sehemu ya pendekezo la kumsajili upya Neymar kurudi Barcelona kutoka Paris St-Germain, bingwa wa Uhispania inaarifiwa walikuwa tayari kutoa Euro milioni 100 na kujitolea Coutinho kumsajili kiungo huyo wa mbele.

Tottenham ilikatiza hamu ya kufikia mkataba wa mkopo kwa mchezaji huyo mapema mwezi huu, wakati amehusishwa pia na uhamisho kwenda Arsenal na kurudi Liverpool.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad