Bobi Wine : Ashtakiwa kwa kumkasirisha na kumkejeli rais Yoweri Museveni


Mbunge wa Uganda na mwanamuziki Bobi Wine ameshtakiwa kwa lengo la kumkasirisha, na kumkejeli rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Mbunge huyo na wenzake wametuhumiwa kwa kuurushia mawe msafara wa rais wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji wa kaskazini wa Arua 2018.

Shtaka hilo jipya limeongezwa katika shtaka jingine la uhaini dhidi ya mbunge huyo.

Wine na wenzake wengi wanasema kwamba waliteswa wakati walipokuwa kizuizini, kitu ambacho mamlaka imekana.

Wine ambaye jina lake ni Robert Kyagulani bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyengine kwa kuongoza maandamano dhidi ya sheria inayoweka kodi katika mitandao ya kijamii pamoja na biashara zinazofanywa kupitia malipo ya simu za rununu 2018.

Msanii huyo ambaye amekuwa mwanasiasa wa upinzani anayepinga utawala wa miongo mitatau ya rais Museveni hivi majuzi alitangaza kwamba atawania urais katika uchaguzi wa 2021.

Tayari amezindua kikosi kitakachoendesha kampeni yake ya kuwania urais 2021.

Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kama changamto kwa Yoweri Museveni.

Museveni, mwenye umri wa miaka 74, anatarajiwa kuwania muhula wa sita madarakani.

Msanii huyo anakabiliwa na mashtaka ya uhaini baada ya kukamatwa mwaka jana kufuatia kupurwa mawe msafara wa rais baada ya mkutano wa kisiasa.

Aliliambia gazeti la Financial Times kwamba zaidi ya wabunge 50 , ikiwemo 13 kutoka kwa chama tawala cha rais Museveni cha National Resistant Movement NRM waliunga mkono ugombeaji wake na hivyobasi kumpatia ujasiri wa kuogombea kiti hicho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad