Bobi wine ataja majina 30 ya walioshikiliwa katika nyumba za mateso

Kamati ya bunge ya haki za bindamu imemtaka waziri wa usalama wa taifa nchini Uganda Jenerali Elly Tumwine kutoa maelezo kama nchini Uganda kuna nyumba za mateso zinazojulikana kama Safe House.

Hii ni baada ya mbunge ambaye ni msanii Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kuifahamisha kamati hiyo jinsi serikali inavyowatesa watu na zaidi wana siasa wa upande wa upinzani katika nyumba hizo.

Waziri huyo wa usalama Jenerali Elly Tumwine amekiri kuepo kwa nyumba hizo na kudai kuwa huwa zinazotumiwa kwa njia ya kiintelijensia, "Hata mimi mwenyewe siwezi kufahamu ni nyumba ngapi zinazotumiwa na vikosi vyote vya ujasusi nchini Uganda.


Nyumba za safe house zipo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa siri na hivyo haziwezi kufahamiki, zipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kina, upelelezi haufanywi hadharani, upelelezi unafanywa kwa siri hivyo unawaita watu sehemu ya siri , na kuanza kufanya upelelezi zipo kwa kupata maelezo ya siri na maelezo ya faida, na huwa wanafahamishwa,"Tumwine alifafanua.

Lakini kwa nini 'Safe house' zinatuhumiwa kutoa mateso makali kwa watuhumiwa?

Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ambaye ni mbunge aliyepo kwenye kama kamati hiyo ya haki za binaddamu alihoji kwa nini nyumba hizo zinawalenga wafuasi wa upinzani?

"Kwa nini wengi wanaokamatwa ni wafuasi wa wanasiasa wa upinzani, hao ndio wamelengwa na ndio wanapotea, wanateswa na kuuwawa?"Bobi Wine alihoji.

Jenerali alipinga vikali shutuma hizo na kudai kuwa kama kuna mtu ana ushaidi wa kuwa nyumba hizo zinawatesa na kuuwa watu basi wanapaswa kutoa ushaidi lakini hakuna anayeweza kuwapeleka kuona nyumba hizo zilipo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad