Breaking News: Wananchi Waandamana DAR Wakitaka Ndege – Video



UMATI wa watu umejitokeza leo Agosti 28, 2019, nje ya ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar, uliopo kwenye Barabara wa Shabani Robert jijini Dar es Salaam, wakishinikiza mahakama ya nchi hiyo iache huru ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) inayoshikiliwa nchini Afrika Kusini kufuatia kesi ya fidia inayomhusu mtu ajulikanaye kama Hermanus Steyn wa nchi hiyo na Serikali ya Tanzania.



Watu hao waliofika kwenye ubalozi huo asubuhi, bila kumtaja kiongozi wao, wamefika kwenye ubalozi huo wakiwa na mabango wakiimba ‘tunataka ndege yetu’. Hata hivyo, polisi walifika eneo la tukio na kuwatawanya watu hao kwa maeleza kuwa, wamefanya mkusanyika na maandamano isivyo halali.


Taarifa ya kukamatwa ndege hiyonchini Afrika Kusini, ilitolewa na Dk. Leonard Chamuriho, katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano tarehe 23 Agosti 2019. Ndege hiyo ya ATCL aina ya Airbus A220-300, ilizuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg mwishoni mwa wiki iliyopita kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng nchini humo.


Hata hivyo, Dk. Chamuriho hakueleza sababu ya kushikiliwa kwa ndege hiyo. Baadaye msemaji wa serikali, Dk. Hassan Abbas kwenye taarifa yake alieleza kuwa, mkulima mmoja ambaye ni mdeni wake alipata amri ya mahakama kuu ya Gauteng, jijini Jonesburg kuzuia ndege hiyo kuondoka.



Baada ya ndege hiyo kushikiliwa, serikali ilituma jopo la wanasheria nchini Afrika Kusini likiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi,  kufuatilia suala hilo ili ndege hiyo iachiliwe haraka na kuendelea na safari zake kama kawaida.



Updates: Watu watatu wanaodaiwa kuwa viongozi walioanzisha maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania inayoshikiliwa nchini Afrika Kusini wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha. Pia, jeshi hilo pia limewatawanya waandamanaji hao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad