Meya wa Manispaa ya Bukoba, Chief Karumuna amesema kuwa kipindi cha mwaka 2010 adi 2015 Manispaa ya Bukoba ilikuwa kichwa cha mwenda wazimu ambapo madiwani wake walikuwa wakirumbana na kupigana.
Hali ambayo ilipelekea fedha za miradi ya maendeleo zilizokuwa zimetolewa na benki ya dunia kurudishwa na hatimaye maendeleo katika manispaa hiyo kukwama.
Chief Karumuna amesema hayo wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Hamgembe katika mkutano wa adhara wa Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini, Willifred Lwakatare. Ambapo amesema kuwa zaidi ya Sh. Bilioni 18 zilirudishwa kutokana na uongozi wa Jimbo kutokuwa na uaminifu katika kusimamia miradi ya maendeleo na kukalia kulumbana bila kutimiza wajibu wao.
"Lakini baada Chadema kuchukua Jimbo hilo Benki ya Dunia imetupa Bilioni 7 baada ya kuridhishwa na uongozi wa chama hicho na sasa Bukoba inaenda kuwa kama Ulaya."
Bukoba Palikuwa Kichwa cha Mwenda Wazimu - Meya Chief Karumuna
0
August 08, 2019
Tags