Bunge la India Kuidhinisha sheria Mpya Kuhusu Kashmir

Bunge la India Kuidhinisha sheria Mpya Kuhusu Kashmir
Bunge la India litaidhinisha mswaada wa sheria utakaobatilisha kanuni za sehemu ya jimbo la Kashmir inayosimamiwa na India katika milima ya Himalaya. Pakistan nayo inajiandaa kuitisha maandamano kupinga uamuzi wa India.

Serikali ya wahindu wanaopigania uzalendo, inayoongozwa na waziri mkuu Narendra Modi imewasilisha mswaada wa sheria kuhusu muundo mpya wa jimbo la Jammu na Kashmir katika bunge la Lok Sahba, siku moja baada ya hatua zilizochukuliwa sambamba na amri iliyotiwa saini na rais ya kubatilisha kifungu maalum kinachodhamini utawala maalum wa ndani katika jimbo hilo.

Hali si bayana katika jimbo hilo baada ya serikali kuzifunga njia zote za mawasiliano na ulimwengu wa nje, ikiwa ni pamoja na internet, simu za mkononi na nyenginezo.Serikali iemtuma maelfu ya wanajeshi katika eneo hilo linalopakana na milima ya Himalaya kwa hofu ya kuzuka machafuko.

Bunge linatarajiwa kuidhinisha bila ya shida yoyote mswaada huo wa sheria unaobatilisha kanuni za jimbo la Kashmir na kuligeuza kuwa jimbo la kawaida, sawa na majimbo yote mengine ya India.

Baraza la Senet limeidhinisha mswaada huo kwa wingi wa thuluthi mbili baada ya wawakiilishi wengi wa upande wa upinzani kuwaunga mkono wawakilishi wa chama tawala cha Bharatiya Janata Party.

Wasi wasi umetanda katika eneo la mpakani linaloigawa Kashmir kati ya India na Pakistan, ambazo zote kila moja inadai Kashmir ni sehemu ya ardhi yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad