CCM,CHADEMA wazidi kutunishiana misuli Njombe

 

Na Amiri kilagalila-Njombe 


Wakati vyama vya siasa vikiendelea kujiimarisha kabla ya kuanza uchaguzi wa serikali za mitaa mapema Novemba mwaka huu,Chama cha mapinduzi CCM pamoja na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Njombe vimeendelea kujitokeza na kutambiana hakuna atakayemshinda mwenzie katika chaguzi hizo hususani katika mitaa iliyopo Njombe mjini inayoongozwa na CHADEMA. 




Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa Chadema mkoa wa Njombe Alatanga nyagawa amesema wanaamini wataendelea kushinda katika maeneo ya mijini ambako bado wanaongoza hadi sasa licha ya kuwapo kwa figisu kubwa za chama cha mapinduzi zinazofanyika katika kipindi cha uchaguzi. 


 “Hapa mjini mshindani wetu sio CCM labda kizaliwe chama kingine,sisi tuna mtaji mkubwa hapa kwa asilimia kubwa wenzetu wameshachoka labda waende sehemu nyingine,sahizi tunachohangaika ni nani asimame kwa mazingira ya sasa kwasababu ushindani mkubwa upo ndani ya chama”alisema Nyagawa. 




Wakati chadema wakijinasibu kuendeleza ushindi katika maeneo yote ya mijini chama cha mapinduzi nacho kupitia katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto ngole anasema hakuna mtaa utakaokaliwa na upinzani katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa. 


“Tatizo Chadema ni chama cha fitina,na safari hii atakayefanya mzaha tunafukuza mchana kweupo na kushinda tutashinda CCM ya Magufuri ni ya tofauti”alisema Erasto Ngole 


Diwani wa kata ya Njombe mjini kupitia Chadema Agrey Mtambo amesema ana imani vyama vyote vimejipanga kikamilifu na kutoa wagombea watakaowakilisha vyema vyama vyao huku akiwataka wananchi kujitokeza pindi uchaguzi utakapoanza ili waweze kuchagua viongozi watakao kuwa bora katika maeneo yao 


Novemba 24 mwaka huu ni tarehe inayotajwa kuwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuwachagua wenyeviti wa mitaa,vijiji na vitongoji ambapo watanzania wanahimizwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili wapate fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad