China Yatoa Msaada Wa Vifaa Vya Ofisini Kwa Ajili Ya SADC


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Wang Ke wamesaini hati za makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya maofisini vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili na kumi na saba kwa ajili ya shughuli mbalimbali za ofisini ikiwemo computer,photocopy na printer kutoka kwa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya mkutano wa SADC.

Katika mkutano huu wa 39 wa Jumuia ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC,Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa kijiti cha uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa SADC.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikabidiana nyaraka za Msaada wa vifaa vya ofisini vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili kumi na saba vitakavyotumika wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa China na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. August 08,2019. na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China hapa Nchini Mhe. Wang Ke

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad