Mchezaji Cristiano Ronaldo anasema licha ya kuwa na upinzani mkubwa na Lionel Messi katika mpira wa miguu mahusiano yao yapo sawa yaani hawana tatizo.
Ameongeza kuwa sio kitu rahisi kwa watu wawili wanaoshindana kusimama kwenye jukwaa moja katika kipindi kisichopungua miaka 15 huku kila mmoja wao akimpa hamasa mwenzake kushindana.
Ronaldo pia amegusia jinsi ambavyo anaakosa kucheza Laliga ambapo wamekuwa na ushindani mkubwa na Messi amekiri pia licha ya ukaribu wao na kuwa na mahusiano mazuri hawakuwahi kujumuika pamoja kwenye chakula cha usiku akitaraji kufanya hivyo kwenye siku za usoni pengine.