“Ndani ya siku saba, hiyo Ultra Sound iwe imenunuliwa na ikabidhiwe kwangu. Siku saba zikiisha mtu hajatoa hiyo fedha afukuzwe kazi. Kama kuna mtu atahoji huko juu anihoji mimi na kama itaonekana nimefanya maamuzi yasiyofaa acha niende nyumbani,” amesema Kiswaga.
Aidha, amesema yupo tayari kufukuzwa kazi kwa kusimamia hili huku akimwagiza Ofisa Utumishi kumfukuza kazi mtumishi yeyote atakayekaidi agizo hilo ndani ya siku saba.
