Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro ameamuru wafanyabiashara wa kumbi za starehe na bar katika jiji la Arusha, kufanyabiashara hiyo bila ukomo wa muda wa kufunga ili kuweza kumudu uendeshaji na ulipaji wa kodi za serikali na mishahara ya wafanyakazi kwa wakati.
Murro ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa bar ya Kanye House iliyopo mkabala na Jogoo house, katikati ya jiji la Arusha na kuwataka weny e bar kuuza vinywaji kwa saa 24 bila kuwa na hofu yeyote kwa kuzingatia kanuni na sheria za uendeshaji wa biashara hiyo.
"Serikali inathanini wawekezaji kama hawa namimi natamka kuwa bar zote zifanyekazi Massa 24 hakuna muda wa ukomo na atakaye wauliza mwambieni DC Muro amesema" Amesema Muro.
Aidha aliwataka wamiliki wa bar kuhakikisha wanatoa ajira rasmi kwa wafanyakazi wao ili kuepuka usumbufu unaotokana na maslahi ya wafanyakazi.
Awali mkurugenzi wa Kanje house, Heladius Kanje amesema kuwa amefungua biashara hiyo ili kuweza kutoa ajiri kwa wafanyakazi na kulipa kodi ya serikali.
Amesema hadi sasa ameajiri wafanyakazi 30 na anatarajia kuongeza idadi hiyo na kufikia wafanyakazi 80 ifikapo mapema mwaka ujao.
Amesema ameamua kuwekeza kwenye bar kwa lengo la kuimarisha soko la vinywaji hapa nchini na kyiwezesha serikali kupata mapato yake kwa wakati na hivyo kukuza uchumi wa taifa.