Diamond arejesha tabasamu la Hawa ‘Nitarejea’


By Nasra Abdallah, Mwananchi nabdallah@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Msanii Diamond Platnumz amezidi kurejesha tabasamu kwa msanii Hawa Said maarufu Hawa Nitarejea  baada ya kupanda naye jukwaani mkoani Dodoma na kuimba wimbo aliomshirikisha wa ‘Nitarejea’.

Diamond anafanya hivyo ikiwa imepita takribani miezi kumi tangu alipomsaidia Hawa matibabu kwa kumpeleka nchini India baada ya msanii huyo kusumbuliwa na maradhi ya tumbo, baadaye kubainika kuwa alikuwa na tatizo la moyo.

Mbali na kuimba pamoja jukwaani, Hawa pia ametoa wimbo ‘Nacheka’ huku akilieleza Mwananchi kuwa wimbo huo ni zawadi kwa mashabiki wake.

Katika wimbo wake huo, Hawa ameeleza nyakati alizopitia, hasa wakati alipokuwa mgonjwa na kuwashukuru wote waliomsaidia mpaka amepona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad