Dk. Bashiru aliyasema hayo wakati alipotembelea majeruhi waliopata ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka mkoani Morogoro.
Alisema kutenganishwa huko kutasaidia magari makubwa kutopita maeneo ya makazi ya watu na hata kukitokea majanga kama ya moto, wananchi hawataweza kupata madhara.
Hata hivyo, aliishauri Serikali kuweka utaratibu wa kutoa elimu ya majanga ya moto ili wananchi waweze kuwa na uelewa mara zote na kuweza kukaa mbali na matukio ya moto ikiwemo yanapoanguka magari ya mafuta.
Mbali kutembelea majeruhi waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, pia alitembelea chumba cha kuhifadhia maiti, kuomba dua makaburini na eneo la Itigi-Msamvu ambako lori hilo lilipinduka kabla wananchi hawajalivamia kuiba mafuta na baadaye moto kulipuka.