DR Congo: Dawa za kupambana na Ebola Zaonesha Ufanisi, Aina Mbili Kati ya Nne Zafanya Kazi Kutibu Ugonjwa Huo

Wanasayansi wameeleza kuwa ugonjwa wa Ebola huenda punde ukadhibitiwa na kutibika baada ya majaribio ya dawa aina mbili zilizoonesha ufanisi.

Mtoa huduma za afya akimchoma sindano ya chanjo mtoto nchini DRC

Dawa aina nne zilijaribiwa kwa wagonjwa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako kuna mlipuko mkubwa wa virusi hivyo.

Dawa aina mbili kati ya nne zimeonekana kufanya kazi vilivyo katika kutibu ugonjwa, utafiti umeeleza.

Dawa hizo sasa zitatumika kutibu wagonjwa wote wa Ebola nchini DR Congo, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Taasisi ya taifa ya utafiti kuhusu uzio na maradhi ya kuambukiza ya nchini Marekani (NIAID), ambao ilidhamini majaribio hayo, imesema matokeo hayo ni ”habari njema” katika mapambano dhidi ya Ebola.

Dawa hizo kwa jina REGN-EB3 na mAb114, zinafanya kazi ya kuvishambulia virusi vya Ebola kwa kuzipa nguvu chembe chembe za kinga za mwili zinazopambana na maradhi.

Ni ”dawa za kwanza, ambazo kisayansi zimeonesha kuwa muhimu katika kupunguza vifo” vya wagonjwa wa Ebola, alisema Daktari, Anthony Fauci, Mkurugenzi wa NIAID.

Dawa nyingine aina mbili ZMapp na Remdesivir, zilishindwa kufanya vizuri kwenye majaribio hayo.

Matokeo ya majaribio yalikuwaje?
Majaribo, yaliyofanywa na taasisi ya utafiti na kuratibiwa na Shirika la afya duniani, WHO, yalianza mwezi Novemba mwaka jana.

Tangu wakati huo, dawa aina nne zilijaribiwa kwa wagonjwa 700, huku matokeo ya awali kutoka kwa watu 499 wa kwanza yakifahamika hivi sasa.Watoa huduma za afya

Kwa wagonjwa waliopewa dawa aina mbili zilizoonyesha kufanya kazi, 29% waliopewa dawa aina ya REGN-EB3 walipoteza maisha na 34% waliopewa dawa aina ya mAb114 walipoteza maisha, NIAID ilieleza.

Tofauti na, 49% ya waliopewa dawa ya ZMapp na 53% waliopewa dawa aina ya Remdesivir walipoteza maisha taasisi hiyo ilieleza.

Matokeo yanamaanisha kuwa mamlaka za afya zinaweza ”kusisitiza watu kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaweza kupona” ikiwa watapata matibabu mapema, alisema Sabue Mulangu, mtafiti wa magonjwa ya kuambukiza.

Dawa hizi zimekuwa na faida gani?
Akisifu mafanikio ya utafiti, Jeremy Farrar, mkurugenzi wa mfuko wa msaada wa masuala ya huduma za kiafya Wellcome Trust, amesema ”bila shaka dawa hizo zinaokoa maisha”.

Matokeo, Bwana Farrar alisema yanaonesha kuwa wanasayansi wako mbioni kuufanya ugonjwa wa Ebola ”kuzuilika na kutibika”

”Hatuwezi kutokomeza ugonjwa wa Ebola kabisa, lakini tuwe na uwezo wa kuzuia ugonjwa huu kuwa mkubwa katika taifa na ukanda,” aliongeza.

Hisia kuwa Ebola haitibiki, halikadhalika hali ya kutoaminiwa kwa watoa huduma za afya chini DR Congo, kumeathiri juhudi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa.

Kuna matumaini kuwa ufanisi wa dawa hizo zilizotengenezwa na makampuni ya kimarekani, zitafanya wagonjwa wajihisi ”kujiamini wanapotafuta huduma mapema”, alisema Daktari Fauci.

Lakini njia nzuri ya kumaliza mlipuko huo, aliongea, ni ”kwa kupata chanjo inayofaa”. Chanjo ni aina ya dawa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad