Dullah Mbabe Ashinda Ubingwa wa Dunia kwa TKO China

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ jana mchana alifanikiwa kumchapa kwa TKO ya raundi ya 3, Zulipiker Maimaitiali raia wa China na kushinda ubingwa wa Dunia wa bara la Asia ‘WBOAP’ uzito wa kati.

Katika pambano hilo ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa TSSG, Qingdao, China ambalo lilikuwa la raundi kumi, Mbabe amefanikiwa kushinda katika raundi ya tatu kwa TKO.

Mbabe ameshinda pambano hilo ambalo limechezeshwa na mwamuzi wa kati, Sawaeng Thaweekoon huku majaji wakiwa Edward Ligas, Surat Soikraching na Mekin Sumon.

Mbabe ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Nimefanikiwa kushinda ubingwa wa Dunia huku China, namshukuru Mungu, naomba Watanzania wafike kwa wingi uwanja aa Ndege siku ya Jumatatu kuchukua ubingwa ambao wamenituma,”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad