Fatma: Ile Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuhusu janga la moto imeishia wapi?
1
August 30, 2019
Wakili wa kujitegemea Fatma Karume amehoji ile tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusiana na janga la moto iliyotokea mkoa wa Morogoro imeishia wapi.
Fatma aliandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa ” Ile Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuhusu janga la moto # Morogoro imeishia wapi? Nawaza tu,”
Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa aliunda tume ya kuchunguza ajali ya lori la mafuta lililopinduka mkoani Morogoro kubaini kama kuna mamlaka zilishindwa kuwajibika baada ya lori la mafuta kupata ajali.
Majaliwa alisema tume hiyo inaanza kazi na kumpatia ripori ndanj ya wiki ili kuchukua hatua.
“Manispaa kuna kitengo cha zimamoto japo najua walikuja kwa kuzima je walikuja baada ya muda gani? Tumesisitiza umakini na uwasibikaji nasikia tumeokoa mafuta sasa tumeokoa yakiwa yameisha? Nitaunda tume wanijibu haya maswali madogo,” alisema Waziri Mkuu.
Aliongezea kuwa:” Je huo muda ambao walikutana hawa ndugu zetu waliotangulia mbele za haki kwa ajili ya kutoa mafuta ni nani aliwazuia? mimi ninajua trafiki huwa wanakuwa na haraka sana ajali inapotokea nani alihusika kuwazuia,” alihoji Majaliwa
Tags
Anti Fatuma, umedamshi Damshi...!!!
ReplyDeletekichuna chuna mwenyewe.
langi nzuri ya njano sijui ni Cucci au luisi vitoni manake kama ingekuwa chama basi ni kama baba na Ammy.
Au Yanga Dam Damu.