Gari hilo litakuwa linafanya safari zake kati ya Mji wa Blagoveshchensk nchini Urusi na Heihe nchini China Miji iliyopo mipakani mwa nchi hizo mbili.
Mwanzilishi wa kampuni ya UNStudio, Ben van Berkel inayobuni na kutengeneza gari hilo wakati akihojiwa na mtandao wa Dezeen amesema wameanza mipango ya kujenga miundombinu ya gari hilo la kwanza litakalounganisha nchi mbili na tamaduni zao.
Gari hilo ambalo huvutwa kwa nyaya inayozungushwa kwa mota litakuwa linatembea katika njia kuu mbili za Kimataifa kwenye nyaya nne, kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 60 na mizigo yao.