Gari la kwanza Duniani linatembea kwenye nyaya kuunganisha nchi mbili


Gari la kwanza la kimataifa linalotembea kwenye nyaya (cable car) ambalo litakuwa linasafirisha abiria kati ya China na Urusi kwa muda wa dakika nane linatarajiwa kuzinduliwa 2020.
Gari hilo litakuwa linafanya safari zake kati ya Mji wa Blagoveshchensk nchini Urusi  na Heihe nchini China Miji iliyopo mipakani mwa nchi hizo mbili.
Mwanzilishi wa kampuni ya UNStudio, Ben van Berkel inayobuni na kutengeneza gari hilo wakati akihojiwa na mtandao wa Dezeen amesema wameanza mipango ya  kujenga miundombinu ya gari hilo la kwanza litakalounganisha nchi mbili na tamaduni zao.
Gari hilo ambalo huvutwa kwa nyaya inayozungushwa kwa mota litakuwa linatembea katika njia kuu mbili za Kimataifa kwenye nyaya nne, kila moja ikiwa na  uwezo wa kubeba abiria 60 na mizigo yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad