Gor Mahia kumtambulisha Kocha Muingereza leo


Mabingwa wa Ligi ya kitaifa nchini Kenya (KPL), Gor Mahia hii leo wanatarajiwa kumtambulisha rasmi kocha wao mpya Steve Polack kutoka Uingereza.

 Kocha huyo mgeni ataanza kazi mara moja kuandaa timu hiyo kuenda Bujumbura kukabiliana na wenzao wa Burundi kwenye mechi ya kufuzu mashindano ya kombe la CAF.

Polack mwenye umri wa miaka 58 aliwasili nchini Kenya jana anachukua usukani kutoka kwa Mturuki Hassan Oktay ambaye alijiuzulu hivi majuzi akitaja sababu za kibinafsi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad