Hakuna Nishani ya Ndoa, Jipange Kwanza na Epuka Presha za Watu, Wengi Wanalia Moyoni, Ningejua...!!


Nianze kwa kusema ndoa ni kitu chema na inapaswa kuwa sehemu ya amani na sio maradhi wala vita.

Kumekuwa na kitabia kinachokera sana, kila mtu akiona bao hujaoa au kuolewa utasikia unasubiri nini utazeeka, au sijui utaitwa babu au vinginevyo

Ndio sio kitu cha kukimbilia, kitu cha kuiga wala cha kuonyesha watu. usimshangae mtu ukikuta hajaolewa au kuoa kwa muda unaotaka wewe au unaodhani wewe ni sahihi. epuka kumpa mtu presha za ndoa kwa sababu wewe uko huko.

Wengi walio kwenye ndoa wanayajua sana sana waliokurupuka. siri ya wanachokipata wanayo wenyewe. usimshangae mtu akifika miaka 30 hajaoa, ana mipango yake.

Ndoa sio kitu cha kujaribu wa kuiga. ingia kwenye ndoa ukiwa na wito, utayari wa mwili na akili na pia utayariwa uchumi ikiwa kulea matumbo zaidi ya matano mwaka mzima bila kukosa kitu.

Hakuna nishani ya ndoa, kwamba ukikimbilia na kuwahikuoa mapema utapata. ndoa ni kitu cha maelewano ya watu wawili yaani mwanaume na mwanamke ambao wanaona wanaweza kuishi pamoja kwa kusaidia na kuheshimia na kukidhiana tamaa.

Tusipende kuishi kwa mikumbo na pia tusipende kuwalazimisha watu waishi kwa mitizamo yetu au experience zetu. usipende kuwauliza uliza watu kuoa.

Kama mwanaume yuko kamili hawezi kuuambiwa aoe muda fulani wakati yeye mwenyewe anajielewa.

Pia kwa wadada, ndoa inatakiwa kuwa sehemu ya maelewano na amani, usiolewa sababu ya umri umeenda, kama yupo wako atakuja tu.

Ukikurupuka kama unakufa kesho utapata jipu uchungu likusumbue mpaka upate kisukaru na mapresha alafu ufe taratibu kwa mateso makali.

Maisha ni jinsi unavyojipanga. Lazima ujipange na kitu cha muhimu kwenye maisha haya ni kifurahia kila siku ukiwa hai.

Usikubali kuishi kwa kunyanyasika sababu ya umri. ishi kwa furaha maana maisha ni mafupi na ukifa hamna maisha tena. Ishi kwa kufurahia kila siku Mungu anayokupa ili uishi vizuri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad