Halmashauri Zakusanya Asilimia 91 ya Mapato Nchini

Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jaffo amesema Halmashauri zote 185 zimefanikiwa kukusanya sh. bilioni 661.4, ambayo ni sawa na asilimia 91 ya malengo ya mwaka wa fedha 2018/19 ya kukusanya sh bilioni 723, ambapo amesema kuna ongezeko la asilimia 9 na mwaka jana,


huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Dar es salaam zikiongoza kwa mapato ghafi.

Hayo yabamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alipokuwa akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za vyanzo vya ndani vya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Jafo amesema Halmashauri za Wilaya tano zilizoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi(asilimia 171),  Wanging’ombe(asilimia 165), Kilolo (asilimia 150), Misenyi (asilimia 142) huku Mbeya DC ikishika nafasi ya tano kwa kukusanya asilimia 141.

Kwa kigezo cha pato ghafi, Jafo amesema Halmashauri zilizoongoza ni Halmashauri ya jiji la Dodoma (Sh bilioni  71.7), Ilala (Sh bilioni 58.1), Kinondoni(Sh bilioni 34) Temeke  Sh bilioni 33.3), Ubungo Mc (bilioni 18.6) na Jiji la Arusha (Sh bilioni 16.4).

“Katika kigezo ya pato ghafi kwa Halmashauri za mji, Geita inaongeza baada ya kukusanya Sh bilioni 8.02 na Halmashauri ya mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho ikiwa imekusanya Shilingi milioni 257.6"

Ameongeza kuwa Wakurugenzi wote wahakikishe ukusanyaji wa mapato hayo ya ndani, unaenda sambamba na upelekeji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo na mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad