Harmonize aibua hisia za kuondoka WCB


Msanii wa muziki nchini, Harmonize ameonesha mabadiliko ya kuondoa utambulisho wake wa kusainiwa chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Mashabiki wamekuwa na shauku ya kutaka kujua iwapo msanii huyu ameondoka ndani ya lebo hiyo mara baada ya kufutilia mbali taarifa za yeye kuwepo WCB zilizokuwa zikipatikana mwanzo wa ukurasa wake wa Instagram.

Ikumbukwe mwanzo msanii Rich Mavoko kabla ya kutoka WCB alianza kwa kuondoa taarifa za kuwepo WCB kwenye ukurasa wake pia.

Lebo ya WCB ambayo inasimamiwa na msanii Diamond Platnumz hadi sasa ina wasanii watano ambao ni Harmonize, Rayvanny, Lava Lava, Queen Darleen na Mbosso. Hata hivyo wiki kadhaa zilizopita Diamond aliweka wazi kuwa yupo mbioni kuongeza msanii mwingine kwenye lebo hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad